BONYEZA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAPA
MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana
yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri,
huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo
waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la
nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa
alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa
kujitegemea wakiwa 68,806.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni
1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453,
wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika
kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha
tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
YOUNG SCIENTIST NDEMBO
Monday, February 18, 2013
Friday, January 25, 2013
HALI SI SHWARI MKOANI MTWARA.
HALI YA MKOA WA MTWARA SI YA AMANI TANGU MCHANA WA HII LEO NA HALI HALISI NDIO KAMA INAVYOONEKANA KWENYE PICHA HAPO CHINI.
CHANZO: MTWARA YANGU BLOG
CHANZO: MTWARA YANGU BLOG
HAPA NI MAENEO YA STENDI KUU YA MKOA WA MTWARA NA HALI NDIO KAMA
INAVYOONEKANA HAPO WANANCHI WAKIWA WAMEZUIA BARABARA NA KUCHOM MATAIRI.
HII NDIO INAYOSEMEKANA KUWA NI NYUMBA YA MH. MBUNGE WA MTWARA VIJIJINI
BI. HAWA GASIA AMBAYO EMEHARIBIWA NA MAWE NA KISHA KUTEKETEZWA KWA MOTO.
BAADHI YA WANACHI WA MKOA WA MTWARA WAKIWA KATIKA MAPAMBANO HAYO.
INAYOSEMEKANA KUWA NI NYUMBA YA MBUNGE MSTAAFU NA MWENYAKITI WA CCM MKOA WA MTWARA
IKIWA IMWHARIBIWA KW MAWE NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI.
Sunday, November 11, 2012
Sunday, July 15, 2012
WAKENYA KUCHUNGUZA TAARIFA ZA KUTEKWA KWA DOKTA ULIMBOKA
Kenya yachunguza taarifa za aliyemtesa Dk Ulimboka | Send to a friend |
Waandishi Wetu SERIKALI ya Kenya imesema inazifanyia kazi taarifa za raia wake kukamatwa na kufikishwa kortini nchini kwa tuhuma za kumteka na kufanya jaribio la kumuua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka. Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Jeshi la Polisi kutangaza kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa raia wa Kenya, Joshua Mulundi anayetuhumiwa kuhusika na tukio la kumteka, kumpiga na kumtupa Dk Ulimboka katika Pori la Akiba la Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni. Balozi wa Kenya nchini, Mutinda Mutiso, alisema kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam jana kuwa Serikali yake itachunguza uraia na tuhuma zinazomkabili mtu huyo ili kubaini ukweli. “Ndiyo kwanza nimewasili kutoka nje ya nchi…, nitafuatilia kwa makini kupata taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi na mamlaka husika za hapa Tanzania na Kenya ili kupata taarifa ya kweli,” alisema Balozi Mutiso na kuongeza: “Siwezi kueleza zaidi kwa sasa kwani itakuwa naeleza uvumi.” MAT wadai kutoridhishwa Wakati Balozi wa Kenya akisema hayo, Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeelezea kutoridhishwa na hatua hiyo kikisisitiza msimamo wake wa kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi kwa lengo la kuwabaini wahusika na kuchukuliwa hatua stahiki. MAT pia imesema kwamba, inaendelea na mpango wake wa kuandamana, ikibainisha kuwa kesho itawasilisha barua ya kuomba kibali cha kufanya maandamano ya amani Polisi. Imefafanua kuwa malengo ya maandamano hayo yaliyopigwa 'stop' na polisi kwa kile walichoeleza ni sababu mbalimbali za kiusalama na kwamba, madai mengi ya madaktari yamefanyiwa kazi na Serikali. "Nisingependa kuingilia suala la kipolisi kwa ujumla wake, lakini moja ya madai yetu ni kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza tukio la kutekwa, kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Pande kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Dk Ulimboka," Katibu Mkuu wa (MAT) Dk Rodrick Kabangila aliliambia Mwananchi Jumapili jana. TUCTA nao wamo Katika hatua nyingine, Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (Tucta) limelipongeza Jeshi la Polisi kwa kumkamata mtu anayedaiwa kumteka na kumpiga kiongozi wa mgomo wa madaktari, Dk Steven Ulimboka. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolaus Mgaya alisema kuwa, hatua ya kumkamata mtuhumiwa huyo inaleta matumaini ya kuwabaini watu wengine waliohusika na vitendo hivyo, jambo ambalo linaweza kurahisisha uchunguzi. Alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linatakiwa kuendelea na uchunguzi ili waweze kuwabaini wahusika wengine na kubaini ukweli kuhusu tukio hilo ambalo limesababisha kutokea kwa hisia tofauti katika jamii. “Tunaliomba Jeshi la Polisi liendelee na uchunguzi ili waweze kuwabaini watuhumiwa wengine na kuwachukulia hatua za kisheria,” alisema Mgaya. Mkenya kukamatwa Joshua Mulundi, ambaye anatuhumiwa kumteka na kumtesa Dk Ulimboka alikamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi alasiri na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya. Wakili Komanya alidai mahakamani hapo kuwa, Mulundi ambaye makazi yake ni Murang'a nchini Kenya mnamo Juni 26, mwaka huu akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk Ulimboka. Hata hivyo, kumetokea utata wa jina, umri wake na makazi ya mtuhumiwa huyo. Wakati hati ya mashtaka mahakamani inasema ni Joshua Mulundi mwenye umri wa miaka 21, mkazi wa Murang’a nchini Kenya, taarifa ya Jeshi la Polisi imesema anaitwa Joshua Mahindi mwenye miaka 31 na mkazi wa Namanga nchini Kenya. Katika shtaka la pili, Wakili Komanya alidai kuwa tarehe hiyohiyo mshtakiwa alifanya jaribio la kumsababishia kifo Dk Ulimboka kwa kumpiga katika eneo la Msitu wa Pande eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria. Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo akidai kuwa makosa aliyoshtakiwa nayo siyo sahihi. Hakimu Mkazi, Agnes Mchome alimwambia kuwa hatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, isipokuwa Mahakama Kuu pekee. Afya ya Dk Ulimboka yazidi kuimarika Akizungumzia hali ya Afya ya Dk Ulimboka anayeendelea na matibabu nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu huyo wa MAT alisema kuwa, Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania anaendelea vizuri na sasa ameanza kufanya mazoezi ya kutembea. "Taarifa tulizonazo sasa ni kwamba, hali ya Dk Ulimboka inaendelea vizuri. Ameanza kufanya mazoezi ya kutembea mwenyewe, anakula na pia anaweza kuzungumza vizuri. Amekuwa akifanya mawasiliano yeye mwenyewe na madaktari wenzake wa hapa nchini ingawa bado kuna matibabu anayoendelea nayo," alisema Dk Kabangila. Mmoja wa Madaktari wa karibu wa Dk Ulimboka aliyepo nchini, alisema Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania amewatumia ujumbe wa kuwashukuru wanataaluma wenzake na Watanzania wote waliomchangia na kumwezesha kupata matibabu nchini humo. Hata hivyo alisema kuwa, Dk Ulimboka ameomba suala la tukio lake la kutekwa na kuumizwa lisiwe hoja ya kujadili, badala yake madaktari na wananchi wote wajielekeze kudai haki zao, ambazo Serikali haijazipa kipaumbele. Dk Ulimboka alisafirishwa nje ya nchi Juni 30 kwa ajili ya matibabu kufuatia jopo la madaktari lililokuwa likimtibu likiongozwa na Profesa Joseph Kahamba kudai afya yake imebadilika ghafla na pia angestahili kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya vipimo na matibabu zaidi ambayo hayapatikani hapa nchini. |
Monday, July 9, 2012
VIDEOZ- VODACOM WAJANJA TOUR NDANI YA MTWARA
JOH MAKIN MWAMBA WA KASKAZIN AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
B12 KUTOKA XXL YA CLOUDS FM
FID Q NGOSHA ZE DON ALIFANYA SHOW YA HATARI
DIAMOND-AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
VODACOM WAJANJA TOUR NDANI YA MTWARA
PRESENTER G14 KUTOKA PRIDE FM RADIO
DJ MOSES FROM PRIDE FM,YOUNG MTWEEZ JEMEDARI WA KUSINI.
MSANII KIBEGA KUTOKA MTWARA AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
BAADHI YA WAJANJA WA MTWARA WALIOUDHURIA SHOW BAB KUBWA YA WAJANJA WA VODACOM MKOANI MTWARA.
WAJANJA WA MTWARA
DJ ZERO KUTOKA CLOUDS FM AKIISABABISHA SHOW BAB KUBWA
PRESENTER G14 AKIWA NA DJ ZERO
DJ ZERO
B12 KUTOKA XXL YA CLOUDS FM
MABESTE AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
B12 KUTOKA CLOUDS FM NA G14 KUTOKA PRIDE FM RADIO
NAY WA MITEGO AKIJIANDAA KUPANDA STEGINI
NAY AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
DIAMOND AKIPA KATIKA TOUR BUS KABLA YA SHOW YAKE
MABESTE AKIWA KATIKA TOUR BUS BAADA YA SHOW YAKE
DJ ZERO AKIWA NA B12 WOTE KUTOKA CLOUDS FM ZE PEOPLES STATION
SHETTA A.K.A KING MSWATI AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
JOH MAKINI MWAMBA WA KASKAZIN AKIJIANDAA KUPANDA STEJINI
NGOSHA ZE DON FID Q AKIWARUSHA WAJANJA WA MTWARA JAMAA ALIFANYA SHOW MOJA BAB KUBWA YAN
FID Q AKITETA JAMBO NA B12.
DJ MOSES FROM PRIDE FM,YOUNG MTWEEZ JEMEDARI WA KUSINI.
MSANII KIBEGA KUTOKA MTWARA AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
BAADHI YA WAJANJA WA MTWARA WALIOUDHURIA SHOW BAB KUBWA YA WAJANJA WA VODACOM MKOANI MTWARA.
WAJANJA WA MTWARA
DJ ZERO KUTOKA CLOUDS FM AKIISABABISHA SHOW BAB KUBWA
PRESENTER G14 AKIWA NA DJ ZERO
DJ ZERO
B12 KUTOKA XXL YA CLOUDS FM
MABESTE AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
B12 KUTOKA CLOUDS FM NA G14 KUTOKA PRIDE FM RADIO
NAY WA MITEGO AKIJIANDAA KUPANDA STEGINI
NAY AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
DIAMOND AKIPA KATIKA TOUR BUS KABLA YA SHOW YAKE
MABESTE AKIWA KATIKA TOUR BUS BAADA YA SHOW YAKE
DJ ZERO AKIWA NA B12 WOTE KUTOKA CLOUDS FM ZE PEOPLES STATION
SHETTA A.K.A KING MSWATI AKIWABURUDISHA WAJANJA WA MTWARA
JOH MAKINI MWAMBA WA KASKAZIN AKIJIANDAA KUPANDA STEJINI
NGOSHA ZE DON FID Q AKIWARUSHA WAJANJA WA MTWARA JAMAA ALIFANYA SHOW MOJA BAB KUBWA YAN
FID Q AKITETA JAMBO NA B12.
Tuesday, July 3, 2012
Fid Q feat Yvonne Mwale - Sihitaji Marafiki official video
Fid Q feat Yvonne Mwale - Sihitaji Marafiki official video
Friday, June 29, 2012
PICHA NA VIDEO ZINAZOONYESHA HALI YA DOKTA ULIMBOKA
Dk Ulimboka akiendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha mifupa (MOI) kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
Tuesday, June 26, 2012
Tuesday, June 19, 2012
MSIMAMO WA MH.MNYIKA BAADA YA KUTOLEWA BUNGENI
Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni!
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!
John Mnyika
19 Juni 2012
FREEMASON NA UONGOZI NA VIONGOZI WA TANZANIA
Sir Andy Chande akiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Andy Chande akiwa na Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.
...Andy akiwa na Mzee Mwinyi.
...Chande na Karume.
....Chande na Sumaye.
HABARI NA GLOBAL PUBLISHERSTZ.JAMII ya Siri (Secret Society), Freemason, imedaiwa kuwa na siri nzito na viongozi wakuu wa nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Madai hayo, yametokana na kile kinachoonekana kwamba Kiongozi Mkuu wa Freemason, Afrika Mashariki, Sir Andy Chande, amekuwa akijiweka karibu na viongozi wakuu wa nchi hii kila awamu, hivyo kuonesha kuwa kuna kitu anakitafuta.
Kikubwa kinachodaiwa ni kuwa Chande anatumiwa na Freemason kuhakikisha kwamba kila kiongozi wa nchi hii anakuwa karibu na jamii hiyo ya siri.
Inazidi kudaiwa kuwa Freemason inafanya njama za hali ya juu kujiweka karibu na Ikulu, ikiwa na mpango wao wa muda mrefu wa kusimika rais ambaye ni memba wa jamii hiyo katika awamu zinazokuja.
Uchunguzi wa Uwazi umeonesha kuwa Chande amekuwa karibu na Ikulu tangu Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na amedumu kujiweka karibu na viongozi wa nchi mpaka awamu hii ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Wakati inabainishwa hivyo nchini, wachambuzi wa mambo ya jamii za siri, ikiwemo Illuminati na Skull & Bones, wamekuwa wakiitaja Freemason kuwa na njama za kuitawala dunia kwa kuhakikisha kwamba kiongozi mkuu wa kila nchi duniani anakuwa memba wa jamii hiyo.
MKAPA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa alipokuwa madarakani aliwahi kualikwa akiwa na mkewe katika shughuli ya Freemasons kutimiza miaka 100 nchini, sherehe iliyojumuisha wageni waalikwa 350 kutoka nchi mbalimbali duniani japokuwa hapa nchini haikutangazwa sana.
Kwa mujibu wa Sir Andy Chande katika mahojiano yake na mwandishi mkongwe nchini, Ernest C. Ambali wa Gazeti la The Guardian, lililokuwa mitaani Oktoba 8, 2004 alitaja waziwazi kuwa mgeni rasmi katika shughuli yao ni Rais Benjamini Mkapa na mkewe Mama Anna Mkapa. Katika shughuli hiyo pia walikuwepo wafanyabiashara wakubwa,wanadiplomasia, mawaziri n.k.
NYERERE
Sir Andy Chande akiwa nchini India katika Mji wa Chennai kuzindua hekalu lao la East Star, alieleza kwamba marais wawili wa kwanza wa Tanzania hawakuwa Freemasons lakini walifahamu taasisi hiyo ni nini na inafanya nini katika nchi hii.
Aidha, aliwahi kuweka wazi kuwa hata Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa akiijua taasisi hiyo na aliwahi kuikingia kifua ilipotaka kunyang’anywa jengo lao ambalo lipo Sokoine Drive, katikati ya Jiji la Dar es Salaam linalofahamika kama Freemasons Hall.
Uchunguzi umeonesha kuwa viongozi wengi wakuu wa serikali wanafahamu shughuli za taasisi hiyo, hali iliyothibitishwa na kiongozi wa Freemasons, Sir Chande ambaye amekuwa akipiga nao picha mara kwa mara wakati wa hafla.
Viongozi wengine wa nchi waliowahi kualikwa au kumualika kiongozi wa taasisi hiyo ni Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye na Rais Mstaafu, Sheikh Ally Hassan Mwinyi.
KITABU CHAKE
Rais mstaafu, Mkapa katika kitabu cha Sir Andy Chande kiitwacho ‘Shujaa wa Afrika, Safari kutoka Bukene’ ameandika utangulizi akisema Chande alikuwa akijulikana kama JK na alifahamiana naye baada ya kumuingiza katika bodi ya Shule ya Shaaban Robert.
Mkapa amesema Sir Chande ametambuliwa na kupewa heshima na vyombo vya taifa na vya kimataifa, heshima ambayo anaistahili kabisa. “Mimi nafurahi kuhusishwa na kutambuliwa kwa sifa na heshima anayopewa,” alisema Mkapa katika maandishi yake.
Mnajimu maarufu nchini, Maalim Hassan Yahya Hussein ambaye amekuwa akiandika makala za Freemasons katika gazeti hili, alipohojiwa na mwandishi wetu kama viongozi hao wanafahamu taasisi hiyo inajishughulisha na nini, alisema japokuwa hakuna anayejua wanachokifanya wanachama wa Freemasons huku uraiani lakini anaamini kuwa viongozi wakuu wa nchi wanajua kila kitu.
“Kwa kawaida huwezi kualikwa katika chama au taasisi fulani bila kujua shughuli zao hasa kwa viongozi wakuu kama hawa, sasa kama waheshimiwa Mkapa, Mwinyi, Sumaye, Karume na Kikwete waliwahi kualikwa au kumualika Sir Andy Chande ni wazi kuwa wanafahamu shughuli zake na taasisi yake,” alisema Maalim Hassan.
KIMATAIFA
Hivi karibuni, nchini Kenya, aliyekuwa Waziri wa Usalama, Profesa George Saitoti aliyefariki kwa ajali ya helikopta, kifo chake kimehusishwa na Freemasons kwa kudaiwa kuwa alipokuwa Makamu wa Rais wa Kenya wakati wa utawala wa Daniel Arap Moi, aliwahi kupiga marufuku makanisa au dini zinazojihusisha na imani za kishetani.
Imeelezwa kuwa wengi wanadhani kuwa angeweza kuwa Rais wa Kenya iwapo angegombea hivyo kurejesha amri yake ya kupiga marufuku imani ambayo yeye haiamini.
Aidha kuna baadhi ya viongozi duniani wanahusishwa na Freemasons baada ya kuonekana picha zao wakionesha alama za taasisi hiyo, baadhi yao ni Rais Barack Obama, George Bush, Sadam Hussein na Muammar Ghaddafi.
Thursday, June 14, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)