BONYEZA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAPA
MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana
yametangazwa. Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri,
huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo
waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la
nne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa
alisema watahiniwa walikuwa 456,137, wa shule wakiwa 397,136 huku wa
kujitegemea wakiwa 68,806.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata daraja la kwanza ni
1,641, wavulana wakiwa 1,073 na wasichana 568, daraja la pili ni 6,453,
wavulana wakiwa 4,456 na wasichana 1,997.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika
kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha
tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa.
No comments:
Post a Comment