Baadhi ya wananchi wa Zanzibar
kwenye kisiwa cha Unguja, wameandamana kupinga muungano kati ya
Tanganyika na Zanzibar inayopelekea kua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maandamano hayo yameleta mchafuko unaoendelea Zanzibar, huku
ikisababisha wakazi wengi wa Unguja kujifungia majumbani mwao wakihofia
usalama wao,huku biashara nyingi zikisimama pamoja na uharibifu wa mali.
Polisi katika kisiwa hicho wanaendelea kufanya jitihada kutulizza
ghasia hizo.
Tutazidi kuwahabarisha yatakayojiri.
Mungu Ibariki Tanzania.
Photo Credits: Aysha Mbarak,Zanzibaryetu.wordpress.com
Tutazidi kuwahabarisha yatakayojiri.
Mungu Ibariki Tanzania.
Photo Credits: Aysha Mbarak,Zanzibaryetu.wordpress.com
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo mtaa wa Kariakoo mjini Unguja limechomwa moto usiku wa kuamkia leo.
Gari la Kiongozi wa
Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Bishop Dickoson Maganga
lililochomwa moto usiku wa jana katika eneo la Kariakoo nje ya kanisa
hilo.
Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU),
kikizunguka katika maeneo ya Michenzani kuimarisha ulinzi ambapo tayari
jeshi la polisi limepiga marufuku mikusanyiko yoyote.
Picha zote na http://zanzibaryetu.wordpress.com/
No comments:
Post a Comment